Kama mtu atakaye isoma Qur-ani kwa nia ya kutafuta radhi za Mola wake, huku yeye akawa anaisoma Qur-ani hiyo kwa makini na kuitafakari vilivyo, basi Qur-ani iatamvuta mtu huyo na kumfanya awe ni mpezi wake wa rohoni. ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Fani ya Fiqhi iliyo katika nyanja za juu (iliyobobea), huwa inampa mtu uwezo maalumu wa kuzivua na kuziopoa hukumu kuu za kisheria kutoka katika machimbuko yake, ambayo miongoni mwayo ni zile ibara za Qur-ani na Hadithi takatifu, na jambo hilo (kuwa na uwezo wa kuziopoa hukumu) ni ...
Kwa mtazamo wa Qur-ani, mwanaadamu ni kiumbe aliyebeba sifa mbili tofauti za kimaumbile, moja ni ile inayotokana na maumbile aliyopewa tokea mwanzo kutoka kwa Mola wake, nayo ni maumbile ya kiroho, na ya pili inatokana na maumbile ya kiwiliwili alichonacho. Maumbile asili ya kiroho (kifitra), huwa ni ...
Tukitoa jawabu ya kiujumla jamala kuhusiana na swali hilo lililoulizwa hapo juu, tunasema kuwa: si katika zama za zamani au za hivi sasa tu, bali katika zama zote hakujawahi kutokea mtu aliyeweza kuja na maneno yenye kufanana na Qur-ani kiufasaha na kibalagha, bali ufasaha unao onekana ndani ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
Uisalmu ni dini kamili iliyokusanya ndani yake mfumo kamili na salama wenye kutoa muelekeo wa kiutendaji kuhusiana na kipengele kimoja kimoja miongoni mwa vile vipengele vinavyo husiana na maisha ya mwanaadamu. Uislamu haukuliweka nyuma suala la afya ya mwili wa kila mmoja wetu. Kwa hiyo Uislamu ni ...
Tukizingatia aina mbali mbali za tafsiri kuhusiana na Aya hii, tutaona kuwa kuna kauli tano tofauti zilizotajwa katika kuifasiri Aya hiyo, na kauli sahihi ni ile isemayo kuwa Aya hii imebeba ujumbe kwa ajili ya walimwengu usemao kwamba: dini ni jambo la kiimani na kimoyo, ...
Jawabu kutoka ofisi ya elimu ya AyatuLlahi Khamenei (Mungu amhifadhi): Iwapo kumfunga huko mimba kutakuwa ni mateso kwa mnyama huyo, basi jambo hilo halitofaa kutendwa. Jawabu kutoka ofisi ya elimu ya AyatuLlahi Mahdi Hadawiy Tehraniy (Mungu amhifadhi), ni kama ifuatavyo: Iwapo ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...