advanced Search
KAGUA
4754
Tarehe ya kuingizwa: 2012/05/20
Summary Maswali
Shakhsiya yake ilikuwa vipi ?mtazamo wa Ahlul bait kuhusiana na yeye.Riwaya zilizonukuluwa kwake zina hukumu gani?
SWALI
Shakhsiya yake ilikuwa vipi ?mtazamo wa Ahlul bait kuhusiana na yeye.Riwaya zilizonukuluwa kwake zina hukumu gani?
MUKHTASARI WA JAWABU
Umayri bni Maliki ni katika wajukuu wa khazraji aliyejulikana sana kwa vinyongo,ni katika sahaba wa mtume,[saww]yeye nikatika kabila la watu wa khazraj na aliishi Madina, alisilimu baada ya kupita miezi kadhaa  ya mtume kufika  Madinah
Abu dardaii aliitikadi ubora wa imamAli[as] dhidi ya Muawiyah.Alifatana na Abu Huraira mpaka kwa Muawiya kumtaaka amtii imam Ali [as]L AKINI Muawiya alileta kisingizio cha kifo cha Othman na kumtaka imamAli[as]aweke wazi sababu za kifo cha Othman.Muawiya akamtuma Abu Dardaii pamoja na AbuHuraira waende kwa imam ALI[as] ili imam aweke bayana sababu za kifo cha Othman,hatima ya jambo hili ni kutokea vita. Wawili hao walifanya jambo hili na walikwenda kwa imamAli[as]Maliki Ashtari alipokutana nao aliwalaumu sana kwa jambo hili kwa siku ile hawakwenda kwa imam Ali [as].Siku ya pili walikwenda kwa imamAli [as] na wakalijadili  swala hili na imam  na walikuwepo watu elfu kumi, na ikathibiti  yeye AbuDardai ni katika watu walioshiriki kumuua Othman kwa hivyo alikata tama na akarejea katika mji wake ,na akawa ni mwenye kulaumiwa na Abdu Rahman bin Othman.
ALakuluhali tunaweza kusema kuhusu yeye kwa mtazamo wa imam ALI[as]yeye ni mfano wa watu ambao”HAWAISAIDII HAKI WALA HAWAIPINGI BATILI”
Ziko riwaya nyingi katika vitabu vya hadithi vya shia na ahli sunah zisemazo Abu Dardaii amenukuu hadithi kutoka kwa mtume [saww]
Baadhi ya wanatarikhi wanasema alikufa baada ya vita vya swiffin,[1]baadhi wanasema alikufa miaka miwili  kabla ya kifo cha Othman
MAJIBU KWA UPANA NA UFAFANUZI
[2]Umayri  bni  Maliki ni katika wajukuu wa Khazraj    [3]NI Sahaba wa mtume kwa sababu ya  kupenda kuweka vinyongo  ndio akaitwa Abu Dardaii .   [4]Yeye ni katika watu wa kabila la Khazraj aliishi Madinah na alisilimu. Kusilimu kwake kulisababishwa na Abdallah bin Rawaha  ambae aliunga nae udugu,Siku moja Abdallah bin Rawah alikwenda nyumbani kwa AbuDardaii na kuanza kuyatusi  ,kuyavunja na kuyapiga masanamu ya ABU DARDAII HUKU AKISOMA SHAIRI LIFUATALO “najilinda na majina yote ya mashetani,na kila ambae atamwabudu Mwenyezi mungu atamsaidia”
Abu Dardaii aliporudi nyumbani kwake mkewe alimuhadithia kile alichofanya Abdallah,AbuDardaii alifikiri kwa muda kisha akasema”ikiwa masanamu yana kheri naweza kuyalinda” hatimae Abu Dardai pamoja na Abdallah walikwenda kwa mtume na akasilimu.  [5]Kwa hakika Abu Dardai hakusilimu baada ya mtume kwenda Madina bali alisilimu baaba ya kupita miezi kadhaa,kitendo cha kuchelewa kwake kuingia katika uislam baadhi ya wanahistoria wamemtaja kuwepo kwake katika vita vya khandak au kutokuwepo kwake katika vita hivyo,na katika vita kabla ya khandak hakuwa muislam. [6] Na katika moja ya vita mtume alimwangalia AbuDardaii na akasema:  ni uzuri ulioje kwa umairy kupanda kipando chepesi chenye uwezo wa kuruka na kwenda kasi .
&nb sp;
[7]Ahli sunah   baada ya riwaya hii wamenakili riwaya nyingine kutoka kwa mtume [saww]isemayo “AbuDardai ni hakimu katika umma wake” [8] na mtume alimuunga udugu na Salman Farsii na wakawa ndugu katika dini.  [9] Uhusiano wake na Salman uliendelea mpaka alipohamia Sham n Salman akiwa Iraq walikuwa wakiandikiana barua. Abu Dardai alimwandikia Salman barua”Hapa nilipo  Mwenyezimungu ameniruzuku mali na watoto na amenipa nyumba katika ardhi takatifu”  Salman akamjibu “umeniandikia una mali na watoto basi jua uongofu hauko  kwa kuzidi mali na watoto”[10] Abu Dardai alikuwepo Madina mpaka katika zama za khalifa wapili alipoamrisha  atolewe Madina na kupelekwa Sham,na khalifa wa pili akamfanya kuwa kadhi. [11]Alipochaguliwa kuwa kadhi watu walisema wamemfurahia nae akasema”mnasema mmeufurahia ukadhi wangu kwa hali  hiyo mmeniweka  chini ya ulinzi ambao kina chake ni kirefu kutoka hapo mpaka kufika pepani.[12]Ikiwa watu wanajua matatizo ya ukadhi na karaha zake wangepeana mkono kwa mkono[wangejiepusha nao] na wangejua kuna malipo gani ya kutoa adhana wangekuwa na shauku na pupa katika hilo na wangenya nga’nyana.[13]Abu Dardai aliitikadi ubora wa imam Ali[as] dhidi ya Muawiyah,yeye na AbuHuraira walielekea kwa Muawiyah kumtaka amtii imam Ali[as] ama muawiyah kwa kisingizio cha kifo cha Othman alimtaka imam aweke bayana sababu za kifo cha Othman na atafute chanzo chake,Abu Dardai na AbuHuraira walikwenda kwa imam Ali[as] kumtaka afanye hivyo njiani walikutana na Malik Ashtar akawalaumu na hawakwenda kwa imam ALI[AS].Ama siku ya pili walikwenda kujadili swala hili na imam pamoja na watu elfu kumi na ikathibiti yeye AbuDardai ni miongoni mwa washiriki wa kifo cha Othman kwa mtazamo huo alikata tama na kurudi mjini kwake na akawa ni mwenye kulaumiwa na Abdurahman bin Othman[14] Uhakika wa kis ahiki utathibiti ikiwa ile kauli isemayo Abu Dardai aliokufa baaada ya vita vya swiffin ,ikiwa tutajengea kama baadhi ya akauli za  wanahistoria alikufa kabla ya utawala wa imam Ali[as]lazima tukubali kisa hiki  hakikubaliki.ala kuli hali kuhusiana na yeye tunasema kwa kauli ya imam Ali[as] kuhusuana na baadhi ya watu”HAWAISAIDII HAKI NA WALA HAWAPINGI BATILI”  [15]AbuDardai kwa mtazamo wa ahli sunah ni katika masahaba wakubwawa mtume[saww] na mwenye hadhi na zimenukuliwa riwaya kutokt kwake.kama ambavyo ziko riwaya chake katika shia zimenukuliwa kutaka kwake kwa mfano shekh Tusii katika kitabu[KHILAF]amenakili fatwa  na riwaya kutoka kwake.   [16] Kuhusu kifo chake kuna maoni tofauti tofautibaadhi ya wanahistoria wanaitikadi alikufa  baada ya vita vya swiffin   [17]wengine wanaitikadi  alikufa miaka miwili kabla ya kifo cha Othman.
 
1;ibn hajar ahmad bin ali bin hajar askalaniial –iswabah fii  tamyizSWahaba juzuu ya 4 ukurasa622 Beirut Darul kitab al-ilmiyah mwaka1415 Qamaria
2]Umayr bni Malik BNI zaidbni Qais bni Umaiyah bni Amir bni ADIBNI Kaab bni Khazraj bni Harith bni Khazraj
[3]Alhashimii Albaswar,Muhammad  bni Saad bni Mani’ii,Altwabaqatil kubra Juzuu ya 7 ukurasa274, Abdul Qair Atwaa,Muhammad, Darul kutub ilmiyah Beirut 1990/1410,Husayn Tafrishii,SayyidM USTAFA, Naqd rijal, Muasasat ali bait[as] Qom chapa ya kwanza 1418 Qamaria
Hakuna shaka kuhusiana nay eye zipo kaulu nyingine baadhi wanaitikadi Amiir ni baba yake wengine  wanaitikadi Amiir ni yeye mwenyewe na alijulikana kama Amir na Umair, nah ii ni katika kitabu cha Ibni  Athiir Abul Hasani Ali bni Ahmad,Asad.
[4]twabaqatil kubra Juzuu ya 7 ukuasa wa 274-275
[5]A bu O mar Yusufu bni abdillah  bni Muhammad bni  Abdul Barr, Al-istiab fii maarifatil  as-hab Juzuu ya 3 ukurasa1228 Darul jiil Beirut 1992-1412
[6]Twabaqatil kubra Juzuuya7 ukurasa274.
[7] Usudul ghabah J uzuuya 5 ukurasa274
[8] hichohicho Juzuu ya 2 ukurasa268.
[9]hicho hicho Juzuu ya 2 ukurasa 268
[10]Bila dhari,Ahmad bni Yahyah, Futuhul buldan, ukurasa204 mtarjuma;Tawakal,Muhammad, Tehran, nashr niqrah mwaka 1337 shamsiyah/ R,K TWABAQATUl kubra Juzuu ya 7 ukurasa275.
[11] Ni miongoni mwa mikoa maarufu nchini Yemen.
[12]Twabaqatil kubrah  Juzuu ya 7 ukurasa 275.
[13Ibni Qutaibah  Dinurii, Abu Muhammad Abdillah bni Muslim,Al-imamaul wa siyasiyah Almaarufu  bitariikh il khulafaa Juzuu ya 1 ukurasa128 Tahqiq ,Shiiri, Ali,Beirut, Darul wudhui ,mwaka 1410 Qamaria
[14]”Hawakuinusuru haki wala hawakuidhalilisha batili”  Imam Ali [as], Nahjul Balaghah, iliyokusanywa na Sayyid Ridhwa,Muswahih: Atwaridii,Azizi llah,ukurasa461, Bun-yad Nahjul Balaghah,BiiJaa chapa ya kwanza mwaka 1372 shamsiyah.
[15]Shekh Tusii,Alkhilaf, Juzuu ya 1 ukurasa 376, ukurasa 380,Juzuu ya 2 ukurasa168,na….. Nashr Jamie  mudarisiin Qom chapa ya kwanza mwaka 1407 Qamaria.
[16]Ibni Hajar Asqalanii,Ahmadbni Ali,Al-iswabah fii tamyiiz swahabah, Juzuu ya 4 ukurasa622, Beirut, Darul kutubil ilmiyah, mwaka 1415 Qamariyah
[17]Usudul ghabah Juzuu ya 4 ukurasa wa20.
TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI